Halibaridi leo -19oC
Tumeamka leo halibaridi imeshuka sana hadi -19oC. Kama picha zinavyoonyesha, hizo barabara kawaida huwa na foleni kubwa asubuhi na jioni, lakini asubuhi ya leo hakukuwa na foleni kabisa. Sababu kubwa mbili. Kwanza watu wengi wako likizo ya Krismasi hadi Jumatatu Januari 4 na pili watu wengi wameamua kuchukua usafiri wa umma kama mabasi na treni za mjini kwenda kwenye mihangaiko yao kwa sababu ya baridi. Barabara nyingi zinateleza.
Watu wengi wanaokaa nje ya Oslo na ambao wanategemea usafiri wa treni za karibu kuja Oslo, wamekumbwa na kusubiri treni zao kwa muda mrefu jana na leo kwa sababu za matatizo ya ishara za umeme kwenye maeneo ya Skøyen, Oslo. Matatizo hayo ya umeme, yamesababisha na baridi kali. Shirika la reli la Norway, NSB liko mbioni kurekebisha matatizo hayo na linategemea kuwa treni zitaenda kiratiba kuanzia alasiri ya leo.

Picha zimepigwa saa 08:00 CET (11:00 EAT)
2 comments:
Poleni mlioko huko Norway!!!!
Dar es Salaam
Poleni mlioko Norway na kote duniani na baridi inayowakumba. Pia kwa wale wanaokumbwa na mafuriko, matetemeko ya ardhi na baharini na wale walioathirika na ukame na njaa na mabalaa mengine duniani...
Dar es Salaam
Post a Comment