Monday, December 07, 2009

New Zealand

Amwambukiza mkewe

UKIMWI kwa kumdunga

sindano akiwa amelala



Jamaa mmoja aliyeathirika, amemwambukiza mkewe UKIMWI huku mkewe akiwa amelala, baada ya kumdunga sindano zenye damu yake mara kadhaa, imefahamika kwenye mahakama moja nchini New Zealand. Mke na mume hao, walihamia New Zealand mwaka 2004 na tayari mume alikuwa ameshaathirika. Mkewe hakuwa ameathirika.

Mke alikuwa mwangalifu, na aliendelea kumpa mmewe unyumba kwa kujikinga. Aliamua kuendelea kuishi na mumewe kwa sababu ya watoto wao. Lakini baadaye mkewe akaingiwa na wasiwasi na kukataa kumpa unyumba mumewe kwa kuhofia kuambikizwa, kitu ambacho kilimwudhi mumewe. Ndipo mumewe alipoamua kumvizia mkewe akiwa amelala na mara kadhaa alimdunga sindano zenye damu yake yenye UKIMWI.

Siku moja mke alishtuka kitu kinamchoma, na kuamka akakuta mumewe ameshika sindano. Mumewe akamwambia kuwa tayari ameshamwambukiza, hivyo hana tena sababu za kumyima unyumba.

Jamaa amekubali kumwathiri mkewe na anaweza kuhukumiwa kifungo cha miaka 14. Jamaa yuko lupango na hukumu yake itatolewa mwakani kwenye mahakama kuu ya Auckland.

Chanzo: Sunday Star Times (New Zealand)

No comments: