Tuesday, December 29, 2009

Norway

Bidhaa iliyotia fora mwaka 2009




iPhone ni bidhaa iliyotia fora kwa mauzo hapa Norway kwa mwaka 2009. Toka ilipoanza kuingizwa kinyemela toka Marekani mwaka 2007 imezidi kuwa maarufu kila kukicha. 


Mauzo rasmi hapa Norway, yalianza 2008 na kampuni ya kwanza kupata leseni toka Apple, ilikuwa ni NetCom. Kwa miezi kadhaa, NetCom ilikuwa na ukiritimba (monopoly), kabla ya Telenor nayo kupata leseni ya kuuza iPhone.


Japo simu kama HTC, Blackberry, Samsung, Nokia, SonyEricsson, n.k. zimekuja na simu zenye vikorombwezo kama iPhone, bado iPhone inaongoza kwa umaarufu. iPhone imekuwa zawadi namba moja kwenye Krismasi ya mwaka 2009.


Mauzo ya iPhone hadi sasa (saa 10.10 CET) ni simu 389,748 kufuatilia takwimu toka iPhonemeter.


Tanbihi:
Fora 
1. Neno linalotangaza ushindi; dungu, goli, ushindi
2. Zaidi ya; bora zaidi


Kutoka kamusi ya Kiswahili Sanifu, TUKI 1996:57

1 comment:

Mosi-O-Tunya said...

Screen touch technology ya iPhone na apps zake kibao ni bab´kubwa!!!

Mtu yeyote aliye na iPhone anakuwa na mapenzi nayo ya aina tofauti kabisa na simu zingine za mkononi.

Hao wengine (Blackberry, HTC, Samsung, Nokia, Sonnyericsson, etc.)wanafuatilia mkia hata wafanye nini. labda waje na mapinduzi ya aina ingine kabisa ya simu za mkononi.

Vinginevyo, iPhone kiboko yao!