CÔte D´Ivoire yaifunga
Taifa Stars 1-0
Juu na chini ni mlinzi wa Taifa Stars Nadir Haroub 'Canavaro' akimdhibiti Didier Drogba wa Ivory Coast wakati wa mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliomalizika muda mfupi uliopita. Ivory Coast walishinda kwa bao lile lile moja lilofungwa na Drogba dakika ya 39. Hata hivyo Taifa Stars, iliyokuwa ikishangiliwa kwa nguvu na mamia ya washabiki wakiongozwa na JK aliyekuwapo uwanjani, wanastahili kila aina ya sifa kwa kuweza kuwamudu Ivory Coast. Canavaro alimzima kabisa Drogba sema walijipanga vibaya wakati Emerse Fae alipochoropoka na kuporomosha majalo.
Picha na habari kwa hisani ya
No comments:
Post a Comment