Thursday, January 07, 2010

Trondheim, Norway

Kakaa na mkasi mwilini wiki 10 baada ya operesheni


Mkasi wenye sentimita 13,4 umekaa mwilini kwa mama mmoja aitwaye Hildegunn Olsens (pichani) kwa wiki 10 baada ya kufanyiwa operesheni ya saratani ya ziwa kwenye hospitali ya Mtakatifu Olav mjini Trondheim. Baada ya operesheni akaanza kujisikia maumivu. Jumanne wiki hii, daktari mpasuaji Knut Holmen wa hospitali ya Lavanger amethibitisha kuwepo kwa mkasi huo kwenye mwili wa huyo mama. Hospitali ya Mtakatifu Olav, wamemwomba mama huyo samahani na watamfanyia operesheni ya kumwondoa huo mkasi.

No comments: