Tuesday, January 26, 2010


Miili yapatikana ajali ya
ndege Beirut


Ndege ya aina ya Boeing 737 ya shirika la ndege la Ethiopia (sio hii iliyoanguka)


Miili ya baadhi ya abiria 90 waliouawa katika ajali ya ndege ya Ethiopia huko Beirut imeopolewa kutoka baharini.

Ndege hiyo iliyokuwa imebeba watu 83 na wahudumu saba ilianguka katika bahari ya Mediterranean.

Ndege hiyo aina ya Boeing 737, ilianguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Beirut nchini Lebanon.

Ripoti zinasema ndege hiyo inamilikiwa na shirika la ndege la Ethiopia.

Watu wanaoishi karibu na bahari ya Mediterranean wameripotiwa kushuhudia ndege hiyo ikianguka baharini huku ikiwaka moto.

Inaaminika kuwa abiria 50 ni raia wa Lebanon huku wengine wengi wakiwa raia wa Ethiopia.

Chanzo: BBC Swahili Service

No comments: