Friday, January 08, 2010

Norway

Kroner 50,000

(T.shs. 11,678,928)
Kumwombe viza jamaa yako



Kama unatarajia kumwalika jamaa yako kuja kukutembelea Norway, basi jizatiti vya kutosha. Kwenye sheria mpya ya wageni iliyoanza kutumika Januari Mosi, mtu yeyote anaweza kutakiwa kuweka amana ya kroner 50 000,- (sawa na shilingi milionikuminamojalakisitasabininananeelfumiatisanaishirininane) kwenye akaunti maalumu. Hiyo ni kama wanamtilia mashaka huyo unayemwalika kuwa anaweza asirudi huko anakotoka. Na kama huyo mtu asiporudi anakotoka basi umepoteza hizo hela. Hayo yamesemwa na Bi. Hanna Krange wa idara ya uhamiaji hapa Norway (Utlendingsdirektoratet)

No comments: