Watu waonywa kutembea kwenye mito,
mabwawa, maziwa na bahari iliyoganda!
Polisi na Zima Moto walifika haraka kwenye eneo la matukio, sehemu za Ulvøya.
Jana watu watatu kwa nyakati tofauti walitumbukia baharini baada ya sehemu ya bahari waliyokuwa wakidhani imeganda kuwa barafu ngumu kuvunjika na wakazama kwenye kisiwa cha Ulv (Ulvøya) maeneo ya Bunnefjordet. Bahati nzuri wote watatu waliokolewa mapema na wamepona. Polisi na Zima Moto zinaonya watu kutotembea kwenye mito, mabwawa, maziwa na bahari wakidhani barafu iliyoganda inahimili uzito wa binadamu.
No comments:
Post a Comment