Friday, April 16, 2010

Bidhaa feki zinazidi kuongezeka nchini Tanzania

Imefikia hata tunaletewa kondom feki!!!


Kondom feki kiasi cha 70,000 zimekamatwa na kutekelezwa na mamlaka ya udhibiti wa viwango TBS (Tanzania Bureau of Standard) na bosi mmoja wa taasisi hiyo Bw. Lazaro Msasalaga amesema nyenzo hizo za ngono zilikamatwa Bandarini Dar kutokea India baada ya kuagizwa na kampuni ya jijini Dar iitwayo Genereics & Specialities Company ambayo ilipigwa faini ya shilingi milioni 3.5 kwa kuingiza bidhaa iliyofaa kwa matumizi ya binadamu pamoja na gharama za uteketezwaji wake. Kondomu hizo, zinazokwenda kwa jina la “Kama Sutra” zimetengenezwa na kampuni ya J.K. Ansell Ltd ya Aurangabad, India ambao unadai kwenye gamba lake kwamba zimejaribiwa kieletroniki na kuridhisha viwango vya kimataifa vya ISO (International Organization for Standardization) na kupewa namba ya uthibitisho 4074 ya mwaka 2002.


Viungo ”links” na CCW oslo.

Kwa marejeo:
Kama Sutra ni maandishi ya kale ya Kihindi pamoja na picha yanayosadikiwa ndio maandishi ya kwanza ya tabia za binadamu kuhusu ngono. Yaliandikwa na mwanafalsafa wa Kihindi aitwaye Mallanaga Vātsyāyana

No comments: