Sunday, April 18, 2010

Blogu ya Ikulu ya Tanzania vipi jamani?


Kuna mtu anaweza kunifahamisha umbumbu wangu wa TEKNOHAMA?.

Hivi blogu ya Ikulu ya Tanzania inaendeshajwe? Haina habari za kila siku…Hivi yote yanayotokea Tanzania, ziara za waziri mkuu hivi karibuni, mama Salma Kikwete, Rais Kikwete safari zake zote za mwezi mzima uliopita, risala zake, hotuba zake, angalau hayo tu yanashindikana kuwekwa kila siku?


Hivi idara ya mawasiliano ya Ikulu hawalioni hili?

Leo Jumapili 18.04.2010. Habari za mwisho kwenye blogu hiyo ni za Machi 18. Mwezi mzima umepita. Matukio mengi yamepita katika kipindi hicho, lakini hakuna hata picha wala nini. Tunaona picha kwenye blogu ya Michuzi, Mjengwa, Hakingowi, Mrocky, Wavuti na nyinginezo za watu binafsi.

Ikulu ka!

Basi wacha blogu, tovuti ya taifa la Tanzania, ndo´kichekesho! Manaake habari haziko katika mpangalio. Ziko shaghalabaghala! Angalieni wenyewe hapo chini


Mbona tovuti za wizara mbali mbali habari zake ziko katika mpangilio? Hii ndio sura ya Tanzania nje ya nchi, lakini mwee…sisemi mengi.

Hata tovuti ya Waziri Mkuu http://www.pmo.go.tz/inapendeza iko katika mpangalio mzuri.

Wenu Tausi Usi Ame Makame,
Oslo



Kopi: balozi@tanemb.se  (Ubalozi wetu nchi za Kaskazini na za Balkani, mjini Stockholm)
Kopi: tanzania@online.no (Chama Cha Watanzania, Oslo)


2 comments:

Jamaaldeen T. Mazar E Shariff Bin Dunia Adonis Ibn Zenjibari said...

Tausi,

Jamaa wako bize na Facebook, Twitter n.k. hawana muda na blogu wanayotakiwa kuifanyia kazi kila siku. Mimi nimeshawaandikia mara kadhaa, lakini mpaka leo hii, sijajibiwa au kuona marekekebisho yoyote!

Ndio nchi yetu ya "Tanza-yenye-nia" inavyoendeshwa.

Sijui hata kama Rais Kikwete anajua kuna blogu ya Ikulu au kuna tovuti ya taifa.

Na kama anajua sijui kama huwa anaipitia angalau mara moja kwa wiki aone tu nini kinaandikwa.

Angeiga mfano wa Rais Barack Obama.

Obama yuko mpka kwenye Facebook na huwa anapitia huko mara kwa mara kusoma nini kimeandikwa!

Washauri wa Rais Kikwete wanamwangusha!!!!

Mosi-O-Tunya said...

Tausi,

Kuna watu wako pale Ikulu hawajui kuwa dunia inabadilika kila siku. Matokeo yake ndiyo kama unayoyaona kwenye blogu ya Ikulu.Usishangae sana! Tena naona wewe si mbumbumbu wa TEKNOHAMA.

Kero yako ni ya maana sana. Naona wataona uliyoyaandika kwani hii nimeiona kwenye:

1. http://www.wavuti.com/
2.http://issamichuzi.blogspot.com/2010/04/blogu-ya-ikulu-ya-tanzania-vipi-jamani.html#comments

Tanzania tunafanya mchezo, wangepitia ya Rais wa Rwanda Paul Kagame waone:

http://www.paulkagame.com/