Saturday, April 24, 2010

Nantes, Ufaransa


Apigwa faini kwa kuendesha
na baibui (niqab/burka)

Mwanamke mmoja wa Kiislam (31) amepigwa na faini mjini Nantes Ufaransa kwa kuendesha gari huku akiwa amevaa baibui. Polisi walimsimamisha mwanamke huyo Aprili 2 na kusema kuwa alikuwa anahatarisha usalama barabarani kwa kuendesha huku akiwa amejitanda uso mzima.

Tukio hilo la Nantes limechukua sura nyingine baada ya waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Brice Hortefeux, kuiamuru idara ya uhamiaji ya nchi hiyo, kumchungumza mume wa huyo mwanamke kwa kusadikiwa kuwa mwanachama wa kundi moja lenye msimamo mkali wa dini ya kiislamu na pia kuwa ana wake wanne, kitendo ambacho ni kinyume na sheria za Ufaransa.

Kama akikutwa na makosa yote hayo, jamaa huyo atanyang´anywa uraia wa Ufaransa alioupata mwaka 1999 kwa kuoana na mwanamke huyo aliyepigwa faini na polisi.

Chanzo: Shirika la habari za Ufaransa, AFP

No comments: