Friday, April 09, 2010

Nimetolewa nje benki ya NBC tawi la Bukoba


Nikiwa nimeamka mapema kuwahi foleni za kila siku za benki, nimekutana na kuubwa leo baada ya kutolewa nje ya Benki hiyo kwa kosa la kuongea na simu na kusoma SMS ndani ya Benki hiyo tawi la Bukoba tumeingia tukiwa wengi ndani ya benki hiyo, na baada ya kufika ndani tukaambiwa benki hiyo haina mtandao hivyo ni vigumu kufanya transactions zetu. 

nikaamua kumpigia simu mdogo wangu niliyekuwa namtumie pesa za shule kama anajinsi, anitumie namba ya Acc katika benki nyinginezo ndipo akatokea mlimzi aliyevalia mavazi ya bluu na kuniambia kuwa nisiongee na simu nikiwa ndani ya benk yake nami nikamueleza kuwa mteja ni mfalme.mlinzi huyo akasimama mlangoni akiniangalia kwa makini hukuakiniahidi kuwa nitaona. 

nikaamua kuitoa simu yangu mfukoni ili niizime, ghafla akaja askari mwenye Bunduki aliyevalia mavazi ya kikosi cha kutuliza ghasia FFU na kuniambia nitoke nje, akaniambia kanifukuza kwa leo ni niondoke, sikumwelewa. akaanza kuniambia kuwa niondoke, nami nikataka nimwone mtu anayehusika na huduma kwa wateja katika benki hiyo ili nimwelize shida yangu na yeye anieleza juu ya taratibu hizo, mlinzi huyo akakataa na kuniamuru niondoke.

Benki hi nimekuwa nikikutana na vikwazo visivyo vya kuwaida na labda ndio taratibu zao. majuzi nikiwa namtumia mdogo wangu ela, nilisahau kuandika namba ya mwisho ya akauti yake, mdada aliyenihudumia alinifukuzia mbali na kufuta (cancel) form zangu kwamba nisimsumbue, kuangalia vizuri ndo nikagundua kuwa kuna namba inakosekana. nikajaza form nyingine na kumpa akaingiza mhamala ule, yaani alishindwa kuniambia juu ya kukosea kwangu kwa kusahau namba moja wapo ambaye ningeijaza na na kumalizia mhamala ule

pia niliwahi kuingia benki hiyo kwa lengo la kuulizia taratibu na kanuni za kufungua akaunti ya kampuni, mwanadada aliyekuwa kwenye dawati la maulizo aliniambia yuko bize na hivyo nirudi baadaye, nikamuuliza kama yeye yuko bize hakuna mwingine wa kunisaidia?? akaniambia nirudi tu baadaye. 

niliporudi majira yamchana akaniambia yuko bize bado ila akaniambia kuna mambo mengi ya kufanya likiwemo kwenda kwa mwanasheria nk, mimi nikamsihi aniambie tu taratibu zote, akaniambia nirudi tu baadaye

nilipopata safariya kwenda jijini Dar es salaam na kwenda katika tawi lao la posta (bila shaka ndo makao makuu ya benki hiyo) ilinichukua muda ya dakika kama mbili tu kupewa maelezo yale abayo ni rahisi tu kuelezeka na kufuatwa, nilishangaa nikabakia na swali kwamba nikifungua akaunti hiyo tawi la Bukoba nitaiendeshaje?

sasa kama kusoma SMS ni kosa ndani ya benki tutafanyaje katika Benk hizi za kisasa zinazokushauri kufanya baadhi ya mihamala kwa njia ya SMS, internet na hata ATM? je, kama namba ya akaunti ya yule ninayemtumia iko kwenye simu ni kosa kuifungua na kuisoma ili niiandika kwa usahihi?? je Benki zenye foleni ndefu na za kukaa muda mrefu ukisubilia huduma, inakuwaje usiomgee na simu kwa lengo la kuweka mambo sawa ofisini kwako au nyumbani au hata kama unasubiliwa na mgonjwa hospitali ili ulete pesa apate vipimo?

lakini je, mimi kama mteja, kwa nini nisiruhusiwe kuonana na mhusika wa huduma kwa wateja ambaye kimsingi yupo kwa ajili yangu???

leo nimekutana nalo hilo benk ya NBC tawi la Bukoba

No comments: