Tuesday, April 06, 2010

Norway

Pasipoti mpya zenye alama za vidole


Kuanzia leo Norway imeanza kutoa pasipoti mpya zenye sehemu za alama za vidole. Wote watakaoomba pasipoti mpya wanapaswa kukubali alama zao za vidole kuchukuliwa. Sababu kubwa za kutoa pasi hizo, ni ongezeko la kupotea au kuibiwa kwa pasipoti zilizoko sasa na serikali kuhofia kuwa ziko mikononi mwa watu wanaotaka kuingia nchi za magharibi kwa nia moja au nyingine. Pasipoti zilizo na alama za vidole itakuwa vigumu kutumiwa na watu wasiopaswa kuzitumia.

Chanzo: taarifa ya habari ya televisheni ya NRK saa 19:00 – 19:25 Jumanne 06.04.2010


No comments: