Saturday, May 01, 2010

Gari lililoundwa na wanafunzi wa
Chuo kikuu cha sayansi na mazingira,
Ås, Norway


Gari hili linaloenda kwa nishati ya kuhifadhi mazingira, limepewa jina Ecotwin


Wanafunzi tisa wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Mazingira kilichopo Aas (Ås), mkoa wa Akershus, wametumia masaa 8000 kuunda gari linaloweza kwenda kilomita 400 kwa lita ya mafuta ya mchanganyiko wa kuhifadhi mazingira na umeme. Ecotwin ni moja kati ya magari mawili toka Norway yatakayoshiriki kwenye mashindano ya magari yanayotumia mishati ya kuhifadhi mazingira, “Shell Eco Marathon” yatakayofanyika Lausitz, Ujerumani.


No comments: