Monday, May 03, 2010

Tatizo la injini, Volvo
inaweza kujiwasha yenyewe


Volvo zenye lita 2,4, silinda 5, injini za dizeli zinaweza kujiwasha zenyewe au hata kuongeza kasi pasi dereva kujua nini kinatendeka. Hii imethibitishwa na kampuni yenyewe ya Volvo.

Hadi sasa kumetokea matukio 55 duniani kwenye magari ya Volvo, linaandika jarida la Kiswidi ya mambo ya magari,  Teknikes Värld 

Yafuatayo  ni aina za magari ya Volvo yanayoweza kuwa na tatizo hilo hapo juu.


  • XC 60 yaliyotengenezwa 2009
  • V70 na XC70 ya kati ya 2008 na 2009
  • S80 ya kati ya 2007 na 2009
  • S40 na V50 ya kati ya 2006 na 2010
  • C30 na C70 ya kati ya 2007 na 2010
Jumla yameuzwa magari 158,000 magari ya aina hizo hapo juu duniani kote na hapa Norway yameuzwa 7194.


No comments: