Friday, May 14, 2010

Wiki hii niliona laivu mashindano ya akina kong'ota


Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.


Mpenzi Frank,

Vipi mpenzi wangu?  Waendeleaje na biashara yako?  Mimi bado nakaa hapa kama vile niko rumande kama mtuhumiwa nambari moja wa mgomo.  Chakula kikichelewa dakika mbili tu nashutumiwa eti nimeanza mgomo baridi.  Na jana, nilipochelewa sokoni kutokana na kulazimika kusubiri mnene fulani kupita na gari lake nene, kidogo mama bosi aende polisi eti nimetoroka na pesa zake. Kumbe wafanyakazi tukicharuka kidogo tunaogopwa teh teh teh.  Tuone hili sakata litaishia wapi.  Maana naona katika hadithi ile, kong’ota ni waajiri wanaotukong’ota na kutukung’uta kila siku lakini mbayuwayu tuna kasi zetu .....



No comments: