Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.
Uzitoni Street,
Bongo.
Mpenzi wa wapenzi, Frank wangu,
Vipi hali yako wewe uliye mbali na mikumbatio yangu? Mzima kabisa? Mimi mzima ukiacha wazimu wa kukukosa wewe.
Nilikuwazia sana jana usiku wakati wa mechi ile kati ya mabingwa na Wabongo. Nilikufikiria ukiwa umejibanza mahali ukishabikia kwa nguvu zote. Wewe nawe Bwana. Si ajabu watu wote walihama na kukuachia luninga maana ukianza kupaza sauti ... hata viziwi watakusikia! Laiti bei ingekuwa nafuu kidogo, najua ungekuja mara moja na kuangalia.
No comments:
Post a Comment