Kiwango cha soka kombe la dunia 2010
South Africa vs. Uruguay
Hapa Diego Forlan akifunga goli la kwanza kati ya mawili aliyofunga
Matokeo ya kombe la dunia
Chile vs. Honduras 1 - 0
Swiss vs. Spain 1 - 0
Uruguay vs. South Africa 3 - 0
Waugwana,
Hivi ni mimi peke yangu au wengine pia mmeliona hili. Mpaka sasa hivi kiwango ambacho kimeoneshwa katika mechi za World Cup kwa kweli hakijaniridhisha.
Nakumbuka Kombe la Dunia mwaka 1994, 1998, 2002. Mechi zilikuwa ni za kuvutia mno. Sina uhakika sana na mwaka 1990 na kurudi nyuma kwasababu wa ukosefu wa kuona mechi live kwenye Luninga. Lakini kwa highlight tuu mambo yalikuwa sio mabaya. Mwaka 2006 bado kiwango hakikuwa kibaya kama ambacho kimeoneshwa mwaka huu 2010.
Hivi ninavyoandika mechi ya 16 imeishachezwa. Spain wamefungwa na Uswizi. Jumla kuna mechi 64 kwahiyo tumeishaona robo ya mechi zote. Labda tukiingia kwenye Knockout stage mambo yatabadilika.
Katika timu za Afrika, Ghana ndio imeonesha matumaini, ikifuatiwa na Ivory Coast kidogo, ambao wanatakiwa kuonesha ari zaidi. Katika timu zote, kwa mtizamo wangu Waitaliano ndio wameonesha kiwango kikubwa pamoja na kutoka draw na Paraguay. Mechi ya Italy-Paraguay ndio pekee ambayo naweza kusema imechezwa katika kiwango cha juu. Ambacho ni high tempo kutoka kwenye timu zote mbili. Quick passing, Attacking football.
Kwa wachezaji , so far only Messi lived up to expectations. Na goli la Maicon limekuwa ni highlight ya WorldCup hii likifuatiwa na lile la Tshabalala. Hopefully, Wabrazil wataongeza kiwango katika mechi zinazofuata.
Imeandikwa na Chris kwenye Tanzanet. Imeletwa kwenye blogu na mdau anayejiita Mosi O Tunya
1 comment:
Chris,
mambo bado! Si umeona Waswiss walivyowaumbua Wahispani? Si umeona Uruguay walivyowatia aibu Bafana Bafana? Raundi ya pili kwenye malundi utaona soka la uhakika!!!
Post a Comment