kitandaza soka la kufurahisha na kuitawala mechi, Ghana ilifanikiwa kuanza vyema fainali za kombe la dunia nchini Afrika Kusini kwa ushindi dhidi ya timu ya Serbia ambayo kabla ya mechi ilipewa nafasi kubwa ya kuondoka na ushindi.
Makosa ya beki wa Serbia, Zdravko Kuzmanovic kuunawa mpira ndani ya maeneo ya penalti kwenye dakika ya 84, yalipelekea mchezaji huyo apewe kadi nyekundu na Ghana kuzawadiwa penalti.
Mshambuliaji wa Ghana, Asamoah Gyan hakufanya ajizi kuizamisha penalti hiyo nyavuni na kuipa Ghana goli la ushindi na pointi tatu muhimu.
Awali kabla ya mechi ya Ghana na Serbia, wawakilishi wengine wa Afrika Algeria walionyesha mchezo dhaifu na kukubali kutandikwa 1-0 na Slovenia ambayo nayo haikuonyesha mchezo mzuri.
Algeria vs. Slovenia 0 - 1
Australia vs. Germany 0 - 4
Australia vs. Germany 0 - 4
No comments:
Post a Comment