Sunday, June 20, 2010

Mgomo wa wafanyakazi kwenye
makampuni ya ulinzi waisha


Kwenye saa 6 za usiku kuamkia leo Jumapili, pande zote mbili yaani waajiri wa makampuni ya ulinzi na wafanyakazi walifika makubaliano ya nyongeza za mishahara, hivyo basi kumaliza mgomo uliochukua wiki moja. Hayo yalisemwa na msuluhishi wa migogoro ya wafanyakazi na waajiri, Bi. Kari Gjesteby. Viwanja vya ndege vilivyofungwa kwa kukosa walinzi, vitafunguliwa na usafirishaji wa hela kwenda kwenye mabenki na maduka utaanza tena kuanzia kesho. Karibu wafanyakazi 2500 kwenye makampuni hayo, waligoma kwa kutokubali, kiwango cha nyongeza za mishahara kutoka kwa waajiri wao.

No comments: