Mgomo wa walinzi:
hela kwenye ATM zimeanza kwisha!!!
Mgomo wa wafanyakazi kwenye makampuni ya ulinzi hapa Norway umeanza kuonekana makali yake, kwani tayari kuna ucheleweshaji kwenye viwanja vya ndege kaskazini ya Norway. Uwanja wa Sola, Stavanger tayari umefungwa. Wasafiri wanaosafiri kutumia Oslo Gardemoen wanaombwa kufika uwanjani masaa matatu au zaidi kabla ya safari zao, kwani kumekuwa na upungufu wa walinzi wanaolinda na kupekuwa wasafiri.
Vile vile kumeanza kuwa na upungufu kwenye mashine nyingi za kuchukulia hela (ATM = Automatic Teller Machines. Wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi ya NOKAS yenye asilimia 70 ya usambazaji wa hela kwenye ATM, wako kwenye mgomo na mashine nyingi zimeanza kupungukiwa na hela. Watu wameanza kupagawa na kuanza kuchukua hela kwa wingi kutoka kwenye hizo mashine, wakihofia kukosa hela kabisa, kabla ya likizo ya jumla kuanza Julai Mosi. Watu wanashauriwa kutumia kadi za plastiki badala ya taslimu.
No comments:
Post a Comment