Friday, June 11, 2010

Tafakari ya Babu




Hama Q anena kuhusu maisha ya jela

Hii sio mara ya kwanza kwa Mastar wetu hapa Tanzania kuonja joto ya rumande ama jela, ukiachana na Wajelajela (FM Academia) ambao wao waliitungia hadi nyimbo JELA, Mtu wa kwanza katika muziki wa kizazi kipya kushtua watu kwamba jela ipo alikuwa ni Khaleed Mohammed (TID) ambae alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kabla ya kupata msamaha.. Na wengine waliokumbwa na zahma hiyo ni pamoja na Actress mwenye jina kubwa aliewahi kuwa miss


Inawezekana ulikuwa hulifahamu hili lakini habari ni kwamba Mwimbaji wa PEMBE LA NG'OMBE kutoka bendi ya Dar Modern Taarab ambapo hapo awali alikuwa ni mwanamuziki wa bongo Flavour HAMA Q ameipata joto ya rumande alikokuwa under arrest katika Gereza la Keko hapa DSM kwa muda wa wiki kadhaa na ameachiwa kutoka Gereza la KEKO mwezi uliopita mwishoni kama kwenye tarehe 29 may (kama sikosei). Ambapo kesi iliyokuwa ikimkabili ni kujeruhi.

katika mahojiano leo Hamma Q ametoa hali halisi ya jinsi jela kulivyo ambapo amesema kwamba mtindo wa kulala ni ubavu ubavu na si chali wala kifudifudi ili usichukue nafasi kubwa, na ukitoka tu kwenda kujisaidia nafasi yako imechukuliwa.

Amesema alipokuwa huko amejifunza mambo mengi sana lakini kubwa ni swala zima la kubana matumizi ambapo chupa ya maji inaweza kutumiwa hata kwa siku mbili, na si kubana matumizi kwenye vyakula tu bali hata karatasi ambazo huwa wanatumia kuandika ujumbe na kuutuma kwa ndugu na jamaa zao.. kipande cha karatasi moja anaweza akakitumia hata zaidi ya mara kumi.

Na huko jela kumbe biashara ya kubadilishana bidhaa kwa bidhaa ambayo ilikuwa ikitumika zama za zamani bado inaendelea ambapo ukiletewa chakula unaweza ukabadilishana na mtu kwa chupa ya maji..
hayo ndio maisha ya huko ndani ambapo yeye anasema siku moja jela ni kama mwaka hakuna uzuri kabisa ila anashukuru alivyofika huko kujulikana kwake kulimsaidia kidogo AKASALIMIKA.. masela hawakumsumbua kwa chochote mpaka anaaga jengo hilo lisilokuwa na heri.

Kwa sasa Hama Q ametoa wimbo wake mpya kabisa unaoitwa toto la kiafrika akiwa na bendi yake ya DAR MODERN TAARAB.. hatujui kama utakuwa kama Pembe la ng'ombe ama vipi!!

Kutoka kwa Zamaradi Mketema

No comments: