Tuesday, August 17, 2010

Aliyeiba kroner milioni 90
ajisalimisha mwenyewe polisi




Jamaa mmoja (35) aliyeiba kroner milioni 90 (T.shs. 22,405,916,736.00), leo adhuhuri amejisalimisha mwenyewe kwenye kituo cha polisi cha Grønland mjini Oslo. Jamaa huyo ambaye amekuwa akitafutwa na Interpol, alifika polisi akiwa na wakili wake. Mwezi Julai, jamaa huyo akiwa na mwanamke mmoja aliyejifanya ni milionea, wakiwa na makaratasi bandia ya kuhamisha hela benki na vitambulisho vya bandia, walienda kwenye tawi la Nordea lililopo maeneo ya Tveita na kuhamisha hizo milioni 90 kutoka kwenye akaunti ya mama mmoja tajiri kwenda kwenye akaunti nyingine, na baadaye wakahamisha milioni 60 kwenda kwenye akaunti moja nchini Dubai.

Polisi wamemkamata mfanyakazi mmoja wa benki ya Nordea, tawi la Tveita, mjini Oslo, kwa kushirikiana na wezi wa mamilioni hayo ya kroner.

Hivi kumekuwa na wizi wa namna hii wa wezi kwenda benki na makaratasi bandia na pasipoti batili zilizotengenezwa nje ya nchi, na  kuhamisha hela toka kwenye akaunti za mamilionea wa hapa Norway kwenda kwenye akaunti za nchi za nje.


No comments: