Simu yangu imekwisha chaji ila nataka kuazima chaja ooohh lakini hazi ingiliani. Usumbufu huo utakwisha kuanzia mwakani wakati nchi za ulaya zitakapo anza kutumia aina moja ya chaja kwa simu za mkononi za aina zote. Mpaka sasa makampuni makubwa kama Apple, Motorola, Samsung na Research In Motion watengenezaji wa Blackberry, wamesha saini makubaliano juu ya swala hilo kasoro Marekani.
Kuwa na chaja moja ya simu kwa simu zote za mkononi kutaondoa usumbufu wa kutafuta chaja inayo kubaliana na simu yako tu wakati wahitaji kuchaji na pia itapunguza msongamano wa kuwa na chaja nyingi kutokana na kila simu unayo nunua kuwa na chaja yake, vilevile itawapunguzia watengenezaji wa simu utumiaji wa malighafi nyingi wakati wa matengenezo ya bidhaa zao.
No comments:
Post a Comment