Thursday, September 23, 2010

Mortensrud (Oslo), Oppegård (Follo)

Aua familia yake na kujiua


Jamaa mmoja (41) ambaye alikuwa anatafutwa na polisi kwa kuua familia yake ya watu wanne, amekutwa amejiua akiwa na binti wake wa miaka saba kwenye bwawa la Gjersjøen kwenye maeneo ya Follo, mkoa wa Akershus usiku kuamkia leo, imethibitishwa na inspekta wa polisi, Bi. Hanne Kristin Rohde wa polisi wa Oslo.

Mpaka sasa polisi hawajui jinsi gani mauaji hayo  yalivyotokea, kwa kuwa mwuuaji mwenyewe kajiua. Mara ya mwisho mmoja wa mwanafamilia alikuwa na mawasiliano na familia hiyo, ilikuwa siku ya Jumanne kwenye saa 8 za mchana. Jana Jumatano shule shule ilikuwa na wasiwasi na iliripoti polisi kuwa wasichana wa baba huyo (mmoja darasa la pili na mwingine wa darasa nne), hawakuhudhuria.

Kwenye saa saa 10:15 za jioni, polisi waliingia kwenye nyumba ya familia hiyo, maeneo ya Mortensrud (Oslo) na kukuta mke wa jamaa huyo (37) na mtoto mchanga wa siku 14 wameuawa.

Polisi wakaanza msako mkubwa wa kumtafuta huyo jamaa, baada ya saa moja wakapata taarifa kutoka kwa polisi wa Follo, kuwa kuna msichana wa miaka tisa amekutwa amekufa kwenye ziwa la Gjersjøen (Follo).

Kwenye saa 7 za usiku kuamkia leo, polisi walimkuta huyo jamaa na mtoto wake wa miaka saba wamekufa kwenye bwawa hilo la Gjersjøen, maeneo ya Follo.

Jamaa huyo mwenye asili ya Irani alikuja Norway mwaka 1991, na mkewe anatoka Morokko.

No comments: