Friday, October 15, 2010

Anayetangaza kuwa mwingine ni mgomvi ndiye mgomvi mwenyewe!



Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street, 
Bongo.


Mpenzi Frank,

Mambo vipi mume wangu mtarajiwa, mgombea wa mapenzi yangu aliyepita bila kupingwa? Hakuna hata haja ya kupika kura za maoni.  Hujambo mpenzi?  Mambo vipi huko?  Ipi inaongezeka joto zaidi, hali ya hewa au hali ya siasa? Teh teh teh.


Mimi ni mzima wa afya kama si wazimu wa hao wendawazimu wanaoazimia kutuzimisha kwa kila njia.  Hivi na wewe ulipata na ule ujumbe pia kwenye sms eti mgombea fulani ni mropokaji na mgomvi anayetaka damu imwagike ili mradi aingie Ikulu.  Eti atageuza nchi yetu Somalia.


No comments: