Wednesday, October 13, 2010


Baada ya siku 69 ndani ya mgodi,
Yonni Barios apokelewa
na mke na hawara!


Yonni Barios akiokolewa na kusubiriwa na hawara wake

Wakati wachimba migodi nchini Chile waliokwama ndani ya mgodi kwa siku 69 wakipokewa kwa shangwe na nderemo na ndugu, jamaa na marafiki zao; Yonni Barios (50) alikuta mapokezi mengine kabisa yakimsubiri.

Alikuta mkewe wa miaka 28; Marta Salinas (56) na hawara wake kwa miaka mitano; Susana Valenzuela wakimsubiri.

Mkewe aligundua muda mrefu wakati jamaa akiwa mgodini kuwa, mumewe alikuwa na hawara. Mkewe Yonni alihisi kuna kitu ambacho hakileti mantiki kwani kuna mwanamke mwingine; Susana Valenzuela alikuwa naye kwenye huo mgodi kwa siku nyingi akimsubiri Yonni akiwa ameshikilia bango la kumsubiri. 

Susana amedai kuwa alikutana na Yonni miaka mitano iliyopita kwenye kozi moja ya mambo ya uganga (Yonni ni mganga msaidizi, wakiwa mgodini wenzake walimpachika jina la Dr.House) na alimwambia Susana kuwa na mpango wa kumwacha mkewe.

No comments: