Ikiwa ni takribani siku tatu zimepita tangu REDET kutoa matokeo ya utafiti ya uchaguzi nafasi ya Urais kuwa JK anaongoza, Kampuni nyingine ya kimataifa ya utafiti ya SYNOVATE wametoa matokeo ya utafiti wao kuhusu nafasi ya uraisi ambao imeonesha kuwa iwapo uchanguzi ungefanyika leo, mgombea uras wa Chama Cha Mapinduzi, DK. Jakaya Mrisho Kikwete angepata asilimia 61 ya kura zote. Dk. Wilbroad Slaa wa Chadema yeye angeshika nafasi ya pili kwa kupata asilimia 16 na kufatiwa na Prof. Ibrahim Lipumba ambaye angepata asilimia 5! Aidha, utafiti huo umeonesha pia kuwa kuna asilimia 13 ya waliohojiwa ambao hawakuweka wazi maoni yao na ambao kama watapiga kura leo, JK angeweza kupata asilimia 70, Dk Slaa asilimia 18 na Lipumba asilimia 6.
"Waliobana maoni yao katika swali hili ni wengi sana asiilimia 13% ya wahojiwa wote. Ikiwa watapiga kura ilivyodhihirika hapa basi 70% watampigia Jakaya Kikwete,Wilbroad Slaa 18%, Lipumba 6% wengine 6%," ilismea sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa mchana huu na Meneja wa Synovate Tanzania, Aggrey Oriwo, mbele ya wanahabari ofisini kwake Mikocheni jijini Dar es salaam.

No comments:
Post a Comment