Monday, February 28, 2011

Mwamba ngoma huvutia kwake - Kifo cha Evans

Naona aliyeandika kwenye Kenyans in Norways blog


haelewi maana ya Kiswahili ya kwenda kwenye kilio/msiba na rambi rambi. Angeelewa angeandika tofauti kidogo na alivyooandika.

Kwenda kwenye kilio/msiba haina maana ya kuchangisha pesa tu.

Wengine hatukutoa pesa, lakini tumepika, tumetoa vinywaji na tumehudhuria tu kumpa pole baba mzazi na kadhalika. 

Vitu kama hivi huwezi kuviweka kwenye thamani ya pesa taslimu!!!



Inaonyesha hakukuwa na mawasiliano mazuri baina ya mama na baba mzazi kwenye ulezi wa marehemu kitu ambacho kiliwaweka katika hali ya kutoelewana! Hili suala ni la mama na baba, sisi wengine hatupaswi kabisa kuliingilia. Huu ni wakati wa kuomboleza!!!

AMA KWELI MWAMBA NGOMA HUVUTIA KWAKE!

Ni matumaini yangu kuwa kifo cha Evans kisilete utengano wa utaifa kwa watu wa Afrika Mashariki. Kwani inaonyesha kila mtu anavutia kwake kwenye msiba huu. Tunayoyasikia yanasikitisha. Baada ya kukaa na kuomboleza, watu wanaanza kutupiana maneno!

Tuwape pole wazazi, yaani Martha (mama kutoka Kenya) na Abdul (baba kutoka Tanzania) na Mwenyezi Mungu Amweke Evans Pema..Ameen!

Wenu mwenye masikitiko; Jamaldeen T. Bin Mazar E Shariff Ibn Zenjibari Dunia Adonis.


1 comment:

Anonymous said...

watu wasiosoma ndio wanaweza ku maind mambo ya kiswahili jamani hata siku tatu hazijafika ,ama kweli mavuvuzela ,ogopeni zambi,wewe hata kama umesimangwa si uminye tuu,