Shirika la ndege laajiri wahudumu
waliobadili jinsia
Kutoka kushoto: Nathatai Sukkaset (26), Dissanai Chitpraphachin (24), Chayathisa Nakmai (24) og Phuntakarn Sringern (24). Picha REUTERS.
Shirika moja jipya la ndege nchini Thailand; PC Air limeajiri wahudumu wanne waliobadili jinsia wanaoitwa “ladyboys” nchini Thailand.
Mwanzoni shirika hilo liliweka matangazo likihitaji wahudumu wa ndege wa kike na wa kiume; lakini lilijikuta likipokea maombi 100 toka kwa waliobadili jinsia, na kuamua kuwaajiri hao wanne.
Shirika hilo litaanza safari zake bara Asia mwezi Aprili, mpaka sasa limeajiri wanawake 19, wanaume 7 na waliobadili jinsia 4.
No comments:
Post a Comment