waliweka kamera chooni kinyume cha sheria
Kamera ya kuchungulia watu wakienda kujisaidia chooni.
Pub moja iitwayo Taffes Pub iliyopo Hønefoss (Hoenefoss) imebambwa na polisi kwa kuweka kamera chooni isivyo kihalali. Haya yamethibitishwa na wakili wa polisi wa Nordre Buskerud. Mfanyakazi mmoja wa Pub hiyo aitwaye Heidi Halvorsen anadai waliweka kamera chooni kwa sababu pamekuwa na vitendo cha uuzaji wa madawa ya kulevya, ugomvi uliokithiri viwango na mambo mengine kadha wa kadha ya kihuni yaliyokuwa yanafanyika kwenye choo cha wanaume kwenye Pub hiyo.
Hata hivyo kufuatana na sheria inayolinda haki za watu binafsi (personopplysningsloven) kitendo hicho ni uvunjaji wa sheria na hakiruhusiwi. Hivyo polisi wanataka kuwashtaki wamiliki wa Pub hiyo.
No comments:
Post a Comment