Mikataba ya Mwinyi, Kikwete kufilisi nchi
VIONGOZI walioingiza serikali katika mikataba mikubwa mitatu ya utata, wameliandalia taifa mzigo mkubwa wa madeni yasiyolipika hata katika miaka 50 ijayo, MwanaHALISI limeelezwa.
Wakati Dowans wanadai Sh. 94 bilioni, IPTL wanadai zaidi ya Sh. 248.6 bilioni kwa serikali/TANESCO kuvuruga mkataba wake.
Mikataba yenye utata na inayotishia kuangamiza taifa ni ile ya kuzalisha umeme ya makampuni ya IPTL, Richmond na Dowans iliyosainiwa wakati wa utawala wa Rais Ali Hassani Mwinyi na rais Jakaya Kikwete.
Pamoja na makampuni hayo kukaba koo serikali na kuifikisha katika mahakama na tume mbalimbali za kimataifa za usuluhushi, gharama za serikali kujitetea zinaendelea kuongezeka.
No comments:
Post a Comment