Saturday, March 19, 2011

Mtoto afungwa kamba kama mbuzi
kwa muda wa miaka 15 sasa

 Kijana huo hapa akimvuta mbunge wa viti maalum mkoa wa Tanga Mhe.Amina Mwindau ili amsaidie kufungua kamba aliyofungwa na mama yake mzazi ,Habari utaipata hivi punde

 Maisha ya kijana huyo ambaye amekuwa akifungwa kamba kama mfugo kisa ni kukabiliwa na tatizo la utindia wa ubongo (kichaa)

Mama Akimfunga Kijana Hassan ili kumdhibiti nyumbani kwao Tanga huku Mama Huyu akisema


"... wewe kaka acha tu! huyo ni mkorofi sana hivi ukimfungulia kamba hapa anazunguka mitaa yote ya mji wa Tanga na hapo alipo ana majeraha ya kupigwa na kuchanjwa na nyembe kutokana na ukorofi wake hivi tumeaona njia pekee ni kumfunga kamba na kumchunga kama ng'ombe akiwa malishoni japo na usiku akilala tuna mfunga kamba pale anapolala" alisema mwanamke huyo anayekadiliwa kuwa na miaka kati ya 23 na 25
Hata hivyo anasema mbali ya kufungwa kamba pia kwa upande wa chakula wamekuwa wakimwekea katika sahani yake maalum na kula akiwa amefungwa kamba huku kwa wiki ama mwezi huoogeshwa mara moja.

Alisema kuwa sababu za kufungwa na kutengwa na familia ni kutokana na tatizo hilo la utindio wa ubongo linalomkabili na kupelekea hali ambayo ndani ya familia yao wamekuwa wakiona kama ni aibu kwa kijana huyo kutembea mitaani na tatizo hilo.

Pia alikili kuwa kijana huyo amekuwa na uwezo mkubwa wa kutambua japo hajapata bahatika kupelekwa shule na kuwa sehemu kubwa hata kutamka baadhi ya maneno ameanza kujifunza baada ya kuanzishwa kwa utaratibu wa kumfunga kamba nje ya nyumba hiyo na hivyo kubahatika kujifunza kuongea kwa kusikika kutoka kwa wananchi ambao wamekuwa wakipita eneo hilo.


“Ujue awali tulikuwa tukimfungia ndani pasipo kutoka nje na jua ameanza kuliona sasa ndani ya miaka mitano hii ila awali hakuwa anatoka nje kabisa na kila huduma alikuwa akipewa ndani na siku zote alikuwa ni mtu wa kushinda ndani amefungwa .....kakangu wewe usimwone hivi huyo hapa ukijaribu kumfungulia kamba atazunguka mitaa yote kuingia katika nyumba za watu na kufanya vurugu hadi wenyewe wanampiga na kumchana na viwembe ....kwa usalama wake na kutuepushia aibu tumeona ni vema kumfunga kama ng’ombe wa maziwa hapa katika kamba”

Hata hivyo alisema kuwa kijana huyo amekuwa akifungwa kama na mama yao mzazi kwa maagizo ya baba yao na kuwa zimekwisha fanyika jitihada mbali mbali za kujaribu kumtibu katika hospitali ya mkoa wa Tanga kiasi cha kijana huyo kuanza kupona ila wazazi wake walimkatisha dozi kutokana na kutokuwa na uwezo wa kifedha kwa maana ya kuwa na nauli ya daladala ya kwenda Hospitali mara kwa mara.

“Hapa unapomwona Hasani ni kama amepona kwani hakuwa hivi alikuwa ni zezeta kabisa ila sasa hivi kutokana na kutibiwa ameanza kupona na kuwa na uelewa hata wa kutambua jambo...”

Habari na Picha na Mdau Francis Godwin

No comments: