Kikombe cha Mbagala
Mbagala kaibuka kaka huyo pichani nae anasema kaoteshwa atoe kikombe cha dawa kwa watanzania ili kuwaponya maradhi mbalimbali sugu.
Jamaa huyo ambae alikuwa kondokta wa daladala na kuacha alibadili dini na kuwa muislamu anapogawa dawa hiyo anakuwa na msaafu mkononi japo hajui hata kuusoma.
Kijana huyo anadai hata babu wa Loliondo yupo chini yake....japo wote wametumwa na mungu.
Wakazi wa eneo hilo wameshafika kwake na kupata kikombe ambacho ni maji ya aina mbalimbali ya bomba,mtoni,mvua,ya chupa anasema ndivyo alivyoagizwa na mungu yake si ya kuchemsha mizizi.
Nimekuwa nikijiuliza maswali bila majibu,huko tunakoenda tutanyweshwa mpaka haja ndogo sasa!!!
Wananchi wanapata kikombe!
Kwa hisani ya http://dinamarios.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment