Saturday, May 28, 2011

Basi la Sumry laua 15 papo hapo!

Habari zinasema kuwa waliokufa ajali ya basi la Sumry ni watu 15 huku majeruhi waliolazwa ni 20 . Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Advocete Nyombi ameuambia mtandao huu kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka taili la mbele na mwendo kasi na kupelekea basi hilo kukosa mwelekea na kupinduka. Dereva wa basi hilo ni kati ya watu waliofariki dunia na kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 4.45 usiku. Wakati basi hilo likitokea Arusha kwenda Mbeya .Majina ya waliokufa ktk ajali hiyo na majeruhi utayapata pindi yatakapo tajwa na kutambuliwa

Kutoka  Dar es Salaam

No comments: