Tuesday, May 31, 2011

Norway - watu washauriwa kuacha....

Kula matango kwa muda



Mtu mmoja amelazwa kwenye hospitali ya Sørlandet mjini Kristiansand kwa kushukiwa kushikwa na bakteria aina ya E.coli. Mtu huyo anaharisha damu na yuko mahututi. Taasisi ya afya ya umma(Norwegian Institute of Public Health au Folkehelseinstituttet),na mamlaka ya usalama wa vyakula (Norwegian Food Safety Authority/ Mattilsynet) wametangaza kuwa bakteria hao wamegundulika nchini Ujerumani kwenye matango na inasadikiwa kuwa matango mengi yaliyoingizwa Norway, kutokea Ujerumani na kwingineko yako kwenye masoko siku nyingi. Watu kadhaa nchini Ujerumani na kwingineko Ulaya Magharibi wamekufa kwa E.coli iliyopatika kwenye matango.

Taasisi hii inatoa ushauri kwa watu kuacha kula matango kwa muda hadi hapo watapokuwa na uhakika wa E.coli hii inayosababishwa kwa kula matango.

News from Sweden in English - Swedish woman dies in E.coli case  



No comments: