Hatari ya mgomo wa mabenki kesho
Kwenye upatanishi wa kila mwaka kati muungano wa wafanyakazi wa benki na muungano wa wamiliki unaoendelea, mpaka sasa hakuna suluhisho juu ya maslahi na nyongeza za wafanyakazi wa benki. Pande zote mbili zinatakiwa kufikia makubaliano ifikapo saa 6 za usiku wa leo. Endapo hapatakuwa na suluhisho, basi kuanzia kesho saa 2, wafanyakazi 15552 wa mabenki, wataanza mgomo ambao utaathiri shughuli zote za kibiashara hapa Norway.
Leo hii kumekuwa na misururu ya foleni kwenye ATM watu wakichukua hela taslimu kwa kuhofia mgomo kesho. Baadhi za ATM zimekwisha hela. Hali hii ikiendelea, itaathiri mamilioni ya watu, kwani hakutakuwa na uwezekano wa kutumia kadi za benki kwenye maduka au sehemu zozote zile za biashara!
No comments:
Post a Comment