Gaidi maarufu la Afrika lauawa mjini Mogadishu!
Fazul Abdullah Mohammed a.k.a Daniel Robertson.
Gaidi maarufu la Afrika lililokuwa linasakwa kwa uvumba na ubani, Fazul Abdullah Mohammed limepigwa risasi na kuuawa mjini Mogadishu, Somalia. Mwili wa gaidi hilo, umepewa serikali ya Marekani kwa ajili ya uchunguzi wa DNA. Inasadikiwa Fazul ndiye aliyekuwa kinara wa mipangilio ya ulipuaji wa mabomu kwenye balozi za Marekani mjini Dar es Salaam na Nairobi mwaka 1998 ambapo watu 220 walikufa na wengine 500 kujeruhiwa.
Alipouawa alikutwa na pasipoti ya Afrika Kusini iliyotolewa 13. Aprili 2009 ikiwa na jina la Daniel Robertson. Pia alikutwa za hela taslimu Dala za Kimarekani 40 000,- (arobaini elfu)
Kwenye pasipoti hiyo inaonyesha Fazul a.k.a Daniel Robertson alipitia Tanzania mwezi Machi mwaka huu.
Fazul alizaliwa kwenye visiwa vya Komoro na alikuwa anazungumzia Kikomoro, Kiswahili, Kifaransa, Kiarabu na Kiingereza
Polisi wa Kenya ndio chanzo cha habari za kuuawa kwa Fazul.
No comments:
Post a Comment