Wednesday, August 17, 2011



 Bunge limepata mzungumzaji sahihi wa muziki wa kizazi kipya, Joseph Osmund Mbilinyi Ijumaa iliyopita alithibitisha kwamba yeye ni Sugu, anaijua Bongo Fleva, anayatambua matatizo yanayozunguka na kusababisha mafanikio yamezwe na wachache.

Mbunge huyo wa Mbeya Mjini, akichangia bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo alisema: “Suala la studio ya rais ndiyo Dowans kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya. Mnapotosha nia njema ya rais kusaidia huu muziki, mnamchoresha tu mtaani...


No comments: