Saturday, August 13, 2011

Sheria ni msumeno siyo nusu meno ya kung’ata kushoto lakini siyo kulia


Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.


Mheshimiwa mpenzi,

Au mpenzi aliyeishiwa, vyovyote vile ujue nakupenda. Naam, hata uishiwe namna gani nakupenda. Waache waheshimiwa wadai heshima huku wakitetea mambo ya kitoto, mimi nakupenda na kukuheshimu na uishiwa wako. Au vipi switii! Naona kichwa chako kimeponapona sasa baada ya mkong’oto wa maFF kwa hiyo chunga sana maana sasa nasikia wanataka kutunga sheria ya kuruhusu maFF zaidi. 

Ama kweli napenda sana serikali yetu … serikasi au serifastafasta. Sarakasi ya serikasi. Yaani badala ya kukaa na kupanga mambo ya msingi wanahangaika kutafuta njia yoyote kuwanyamazisha wanaowapinga. Kweli mpenzi. Mara wafukuzwe bungeni, mara wakamatwe na kusafirishwa na ndege ya kijeshi na sasa wanataka kuwaandama wanaoandamana. Hizi kweli si mbinu za mfa maji?....



No comments: