JAMHURI YA MUUNGAN O WA
TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
TAARIFA KWA UMMA
NOTISI YA KUANZISHA MIKOA NA WILAYA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mamlaka
aliyopewa chini ya Ibara ya 2(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
anaweza kuigawa Jamhuri ya Muungano katika Mikoa, Wilaya na maeneo mengineyo
kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Sheria au kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa
na Bunge.
Katika kutekeleza Mamlaka hayo, Rais ametoa notisi ya
kusudio la kuanzisha Mikoa minne (4) na Wilaya kumi na tisa (19). Notisi hizo
ambazo zimetolewa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria ya Uanzishaji wa Mikoa na
Wilaya Sura 397 ya Toleo la 2002 ni Tangazo la Serikali Na. 285 la tarehe 9
Septemba, 2011 kwa ajili ya uanzishaji wa Mikoa na Tangazo la Serikali Na. 287
la tarehe 9 Septemba, 2011 kwa ajili ya uanzishaji wa Wilaya.
Madhumuni ya Notisi hizi ni kuzialika Taasisi na mtu
mwingine yeyote ambaye ataathirika na uanzishaji huo kutoa maoni, mapendekezo
au pingamizi iwapo yatakuwepo katika kipindi cha siku 21 kwa Mikoa mipya na
siku 30 kwa Wilaya mpya kuanzia tarehe ya Notisi hizi.
Baada ya muda uliowekwa kupita, Rais atachambua maoni,
mapendekezo na pingamizi zilizotolewa na kuzitolea uamuzi kabla ya kuanzisha
rasmi Mikoa na Wilaya hizo kwa kadri atakavyoona inafaa.
Mikoa mipya inayoanzishwa na Makao Makuu yake ni kama
ifuatavyo: -
MKOA
|
WILAYA
ZAKE
|
MKOA
ZINAKOTOKA
|
MAKAO
MAKUU
|
|
1.
|
Geita
|
Geita
|
Mwanza
|
Geita
|
|
|
Nyang’hwale(Mpya)
|
Mwanza
|
|
|
|
Chato
|
Kagera
|
|
|
|
Bukombe
|
Shinyanga
|
|
|
|
Mpya/Mbogwe
|
Shinyanga
|
|
|
|
|
|
|
2.
|
Simiyu
|
Bariadi
|
Shinyanga
|
Bariadi
|
|
|
Itilima
(Mpya)
|
Shinyanga
|
|
|
|
Maswa
|
Shinyanga
|
|
|
|
Meatu
|
Shinyanga
|
|
|
|
Busega
(Mpya)
|
Mwanza
|
|
|
|
|
|
|
3.
|
Njombe
|
Iringa
|
Njombe
|
|
|
Wanging’ombe(Mpya)
|
Iringa
|
|
|
|
Ludewa
|
Iringa
|
|
|
|
Makete
|
Iringa
|
|
|
|
|
|
|
|
4.
|
Katavi
|
Mpanda
|
Rukwa
|
Mpanda
|
|
|
Mlele(Mpya)
|
Rukwa
|
|
Wilaya
mpya zinazoanzishwa na Makao Makuu yake ni kama ifuatavyo: -
WILAYA MPYA
|
WILAYA MAMA
|
MKOA
|
MAKAO MAKUU
|
|
1.
|
Buhigwe
|
Kasulu
|
Kigoma
|
Buhigwe
|
2.
|
Busega
|
Magu
|
Mwanza
|
Igalukilo
|
3.
|
Musoma
|
Mara
|
Nyamisisi
|
|
4.
|
Chemba
|
Kondoa
|
Dodoma
|
Chemba
|
5.
|
Gairo
|
Kilosa
|
Morogoro
|
Gairo
|
6.
|
Ikungi
|
Singida
|
Singida
|
Ikungi
|
7.
|
Itilima
|
Bariadi
|
Shinyanga
|
Itilima
|
8.
|
Kakonko
|
Kibondo
|
Kigoma
|
Kakonko
|
9.
|
Kalambo
|
Sumbwanga
|
Rukwa
|
Kalambo
|
10.
|
Kaliua
|
Urambo
|
Tabora
|
Kalua
|
11.
|
Kyerwa
|
Karagwe
|
Kagera
|
Rubwera
|
12.
|
Mbogwe
|
Bukombe
|
Shinyanga
|
Mbogwe
|
13.
|
Mkalama
|
Iramba
|
Singida
|
Nduguti
|
14.
|
Mlele
|
Mpanda
|
Rukwa
|
Inyonga
|
15.
|
Momba
|
Mbozi
|
Mbeya
|
Ndalambo
|
16
|
Nyang’hwale
|
Geita
|
Mwanza
|
Nyang’hwale
|
17.
|
Nyasa
|
Mbinga
|
Ruvuma
|
Mbamba Bay
|
18.
|
Uvinza
|
Kigoma
|
Kigoma
|
Lugufu
|
19.
|
Wanging’ombe
|
Njombe
|
Iringa
|
Waging’ombe
|
Kwa
taarifa hii, Wananchi wote wanaalikwa kutumia haki yao ya kisheria kutoa kwa
maandishi maoni, mapendekezo na pingamizi kama zipo kwa kuzingatia utaratibu
uliwekwa kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi wa maeneo husika na maslahi ya
Taifa kwa ujumla. Maoni, pingamizi au mapendekezo hayo yatumwe kwa kutumia
anuani ifuatayo: -
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa,
S. L. P 1923,
DODOMA.
E-mail hakattanga@yahoo.com
Fax-
026-2322116
Imetolewa na: -
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
9
Septemba, 2011
No comments:
Post a Comment