Jana
nikiwa na darasa langu tulitembelea shule ya Sørkedalen iliyopo maeneo ya
Sørkedalen, Manispaa ya Bærum (Baerum) kwenye mpaka kati ya mkoa wa Oslo na
Buskerud. Madhumuni ya safari - kutembea
kilomita 3 msituni kwa kutumia ramani na dira na kupika kwa kutumia nyenzo za
mapishi za kiasili za Kinorwejiani.
Niliokota jiwe hili. Wanajiolojia wanaliita liitwalo Porphyry.
Jiwe hili
linapatikana maeneo matatu tu duniani: Maeneo ya kuzunguka Oslo, kwenye mlima Kilimanjaro, na
kwenye kontineti la barafu la kusini ya dunia (Antaktika).
Mwamedi
Semboja,
Oslo.
No comments:
Post a Comment