50
Cent akutana na vijana waliopona kwenye
kisiwa
cha Utoya
50 Cent akizungumza na kiongozi wa AUF, Eskil Pedersen baada ya konseti mjini Stavanger.
Alhamisi
wiki hii mwanamziki wa kizazi kipya (Hip Hop/Rap) 50 Cent alitumbuiza kwenye
tamasha la Rått na Råde mjini Stavanger. Baada ya tumbuizo lake, 50 Cents
aliomba kukutana na vijana wa chama cha vijana cha Labour Norway cha AUF,
waliopona kwenye mauaji ya Julai 22 ya vijana wa AUF kwenye kisiwa cha Utoya. 50 Cent pia alizungumza
na kiongozi wa AUF; Eskil Pedersen (24). 50 Cent aliwaambia vijana hao wa AUF
kuwa yuko nao pamoja kwani amekuwa akifuatilia kwa makini tukio la ulipuaji wa majengo ya serikali Oslo
na la mauaji ya Utoya. Aliwaambia pia kuwa yeye mwenye aliwahi kupigwa risasi mara
9 mwaka 2001 na kupona hivyo basi ana hisia na uchungu nao hao vijana.
No comments:
Post a Comment