Marekani
yaruhusiwa kuhifadhi taarifa binafsi za wasafiri wote wa ndege kwa zaidi ya
miaka 15 ijayo!
Pamoja
na upinzani mkubwa kutoka mataifa ya Ujerumani na Austria, mawaziri wa nchi za
Umoja wa Ulaya (EU) wameidhinisha makubaliano kuruhusu idara za usalama za
Marekani kuhifadhi takwimu binafsi za wasafiri wa ndege kwa miaka 15.
Makubaliano
hayo ambayo ni lazima yaidhinishwe na Bunge la nchi za Umoja wa Ulaya, yanatoa
haki kwa mashirika ya Marekani kuchambua taarifa kwa muda wa miaka 15 kwa ajili
ya uchunguzi unaohusiana na ugaidi.
Miongoni
mwa taarifa hizo pamoja na mambo mengine, zinahusu majina ya wasafiri, anwani
zao na taarifa zao za kadi za benki.
Vyanzo:
1 comment:
Duh! Yaani mataifa ya Ulaya hayana ubavu mbele ya Marekani? Aibu kubwa!
Post a Comment