Ufisadi
wa Blandina Nyoni huu hapa!
Kama nilivyohaidi, nimeendelea kuwasiliana na
watumishi wa Wizara ya Afya na wa Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu Ufisadi
wa Blandina Nyoni. Yafuatayo ni baadhi ya vitendo vya Ufisadi vya Mama huyu
ambaye kwa wengine wanamuona kama mchapa kazi hodari
asiyekuwa na doa na anaezuia mianya ya wizi:-
1. Amekuwa akilipwa mshahara wa ziada na Mradi wa
Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP) wakati tayari serikali inamlipa mshahara wa
ngazi ya Commissioner kupita Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
2. Ametengua utaratibu rasmi wa kila Idara ya Wizara
ya Afya kuwa na afisa manunuzi wake badala yake ame centralize kwake mwenyewe.
Kwa maana hiyo, manunuzi yote ya Wizara anamlazimisha (Comand) Mkurugenzi wa
Kitengo cha Manunuzi kumpa kazi zote ndugu yake anaeitwa Donatha Koko.
3. Amekuwa akicomand wizara kununua uniform za
madereva, suti za sikukuu (Sabasaba na Nanenane) na Mauakutoka Mariedo bila
kushindanisha na muuzaji mwingine kinyume na kanuni za manunuzi.
4. Katika mikutano yote inayofanyika Wizarani,
amekuwa akicomand kampuni ya Kaliula Catering Services kupewa tenda ya kulisha
chakula washiriki tangu alipotua Wizarani kama Katibu Mkuu.
5. Miezi mitatu iliyopita aliiteua kampuni ya Soft
tech ambayo yeye ni mbia kwenda kukagua Accounts System ya Muhimbili kinyume na
kanuni za kikaguzi kwa kuwa tayari ana ‘Conflict of Interest’
6. Amekuwa akiongoza Wizara kwa kutumia Informers
ambao kazi yao kubwa ni kumpelekea
habari nani anasema nini na nani anasema nini kuhusu yeye binafsi na uongozi
wake. Informers wake wakuu ni Elias Mkumbo ambaye ni dereva na Donatha Koko
ambeye ni ndugu yake wa damu damu na ni afisa ugavi wa wizara
7. Amemkopesha gari la serikali aina ya Suzuki
Informer wake Elias Mkumbo (dereva) ambae kimsingi hastahili kukopeshwa gari
kutokana na cheo chake. Kwa dereva wa serikali, anachoruhusiwa kukopa ni
Baiskeli, Piki piki na Piki piki ya miguu mitatu (Bajaj)
8. Amenunua vingamuzi vya magari (Fuel control
system) vibovu kwa ajili ya magari manne kwa shilingi 1.3 Billion bila kufuata
taratibu za manunuzi kwa kucomand Single source procurement kutoka kampuni moja
yenye makao yake huko Israel. Manunuzi haya yamefanyika wakati Hospitali nchini zikiwa hazina
dawa, Interns doctors hawajalipwa mishahara yao,
watumishi wake wakidai fedha za likizo, uhamisho na vyuo vingi vya afya vilivyo
chini yake vikiwa na madeni lukuki.
9. Mwishoni mwa mwaka wa fedha 2009/2010 alihamisha
kiasi cha Shilingi 1,968,475,931 mali ya Wizara ya Afya
kwenda National Institute for Medical Research (NIMR) bila kibali cha hazina
kwa matumizi yasiyojulikana. Fedha hizi zilikuja kuhojiwa na CAG katika ripoti
yake ya serikali kuu ya mwaka 2009/2010
10. Mwishoni mwa mwaka huo huo wa fedha alihamisha
kiasi cha Shilingi 3,083,400,000 mali ya Wizara ya Afya
kwenda Health Sector Development Project bila kibali cha hazina kwa matumizi
yasiyojulikana. Fedha hizo pia zilihojiwa na CAG.
11. Amelikosesha Taifa kupata fedha za Mfuko wa
dunia mzunguko wa 11 (Global Fund Round 11) kwa kupitia Mradi wa Taifa wa
kudhibiti Malaria Nchini (NMCP) kwa kushindwa kutumia fedha zote zilizotolewa
na mfuko huo katika mizinguko ya nyuma. Kwa
kifupi ni kwamba Global Fund hawatoi pesa wakiona una Significant unspent
balances.
12. Amekuwa akizuia uhamisho
wa Chief Accountant (Bi Helen Saria Mwakipunda), Chief Internal Auditor (Bi
Anna Joseph Mhere) na Director of Adminstration and Personnel (Bi Tabu Chando)
kwa kile anachodai wanamsaidia katika utendaji wa Wizara. Amezua barua za
uhamisho za Chief Accountant mara mbili, Chief Internal Auditor mara moja na
Director of Administration and Personnnel mara moja. Ukweli ni kwamba amekuwa
akizua uhamisho wa wakurugenzi hawa kwa sababu ni watu waoga na wamekuwa
wakikubali chochote anachosema hata kama kinavunja
kanunu na taratibu za serikali mfano katika maeneo ya Manunuzi.
13. Amemuhamisha aliyekuwa
Kaimu wa Kitecho cha Ugavi Mzee Funga kwenda Hospitali ya Mirembe kwa kukataa
kununua Uniforms, suti na Maua kutoka kwa
Mariedo kwa sababu alihoji ni kwa nini Mariedo watoe huduma wakiwa hawana
Mkataba na hawajashindanishwa.
14. Amekuwa akihama hama na dereva
wake toka Hazina alipokuwa Muhasibu Mkuu wa serikali hadi Wizara ya Maliasili
na Utalii kama Katibu Mkuu. Pia amehama na dereva huyo huyo kutoka Maliasili
hadi Wizara ya Afya kinyume na taratibu na kanuni za Utumishi wa umma ambazo
haziruhusu kiongozi au mtendaji yeyote wa serikali kuhama na dereva au / na
secretary
15. Hamsalimii Naibu wake Waziri
Bi Lucy Nkya kutokana na Naibu huyo kugoma kupangiwa dereva ambaye ni Informer
wake. Hadi leo hii hamsalimii hata wakikutana kwenye kordo. Kinachowazungumzisha
ni madokezo tu.
16. Alikuwa na uhusiano
mbaya na Naibu Waziri wake aliyeondoka Bi Aisha Kigoda kwa sababu ambazo
hazijulikani. Kama ilivyo kwa Lucy Nkya nae pia walikuwa hawasalimiani.
17. Akiwa Wizara ya
Maliasili na Utalii, aligombana na Waziri wake Bi Shamsa Mwangunga na wakawa
hawasalimiani hata wakikutana kwenye kordo
18. Alipokuwa Mhasibu Mkuu
wa Serikali alikuwa anateua ndugu zake na watu anaofahamiana nao na kuwapa vyeo
vya u Chief Accountants na Chief Internal auditors bila kuwa na sifa kamili za
kuhold CPA (T) na Masters.
19. Amesababisha kushuka kwa
morali ya utumishi kwa Wafanyakazi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Hivi
sasa ndiyo Wizara inayoongoza kwa kuwa na watumishi wengi walioamua kwenda
likizo ya masomo ili kuepuka manyanyaso yake.
20. Ameanzisha utaratibu
ndani ya Wizara ya Afya wa kupokea Excheque kutoka hazina na anazihold bila
kufanya distribution kwenye idara zake. Kutokana na utaratibu wake huu anafanya
malipo kwa kutegemea mahitaji yanavyojitokeza. Utaratibu huu ni kinyume na
kanuni za hazina za matumizi ya fedha za umma.
21. Yeye ndiye chanzo cha
masahibu yanayowakabili Watanzania hivi leo kwa kukosa huduma ya afya kwa
kitendo chake cha kutaka kulipiza kisasi kwa Intern Doctors kwa kuwahamishia
Mikoani pale walipodai haki zao ambazo ni stahili zao halali
Imeletwa na mdau
Mosi-O-Tunya
Kutoka Jamii Forums
No comments:
Post a Comment