SUALA
la kuibiwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Adam Malima, si la mchezo
hata kidogo kama kweli tunataka kuheshimu utawala wa sheria na
maadili kwa mtumishi wa umma kama yeye, tena mwanasiasa.
Sasa,
kwa mujibu wa vyombo vya habari, vikimnukuu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Morogoro, hebu tuangalie alichoibiwa waziri huyo:
1.
Laptop tatu, aina ya Dell zenye thamani
ya sh milioni 5.6.
2.
Vinasa sauti viwili vya digitali na
headphone zake zote ambavyo thamani yake ni sh milioni moja.
3.
Simu tatu, ya kwanza Nokia C6 ya sh
500,000, Nokia E200 ya sh 250,000 na Blackberry yenye thamani
ya sh milioni 5.5.
4.
Vitu
vingine ni pete mbili za almasi zenye thamani ya sh milioni 2.5.
5.
Dola za
Marekani 4,000 ambazo ni sawa na sh milioni 6.5.
6.
Fedha
taslimu sh milioni 1.5.
7.
Kadi
mbili za benki.
8.
Mabegi
matatu ya nguo.
9.
Baraghashia mbili zenye thamani ya sh
50,000.
10. Nyaraka
mbalimbali za serikali.
Pia awali ilitajwa na vitu hivi:
11. Pasipoti mbili za kusafiria (zimeokotwa
jalalani karibu na hoteli).
Lakini bahati yake hakuibiwa silaha
hizi, Bastola moja na bunduki iliyotajwa bila aibu kuwa ni SMG (Sub-Machine
Gun).
UCHAMBUZI
RAHISI
1.
Kuna
element ya excessiveness kwenye orodha ya vitu hivi. Kwa maoni yangu
huu ni ulimbukeni kama wa hadithi ya zuzu aliyeshinda bahati nasibu
akaamua kununua kila kitu mtaani kwake, hadi kituo cha basi.
Waziri
kwa mishahara yetu ni mtu maskini labda kama ni mwizi.
Ndiyo,
yeye ni mbunge mwenye maposho, lakini bado alipataje mali zote hizi?
2.
Katika
hali ya kawaida, mwanasiasa anasafiri na laptop tatu za nini?
Huu ni
ulimbukeni wa kujua kompyuta na kuweza kuzipata kirahisi au kupewa
hovyo hovyo tu; vinginevyo nini kinaweza kuwa sababu?
3.
Vinasa
sauti, je, yeye amekuwa mwandishi wa habari au mpelelezi anayetafuta
ushahidi wa sauti? Nini hasa?
4.
Simu
tatu, bahati mbaya ni utamaduni wa hapa nchini Tanzania lakini pia sijawahi
kusikia Blackberry ya gharama zote hizi karibu zaidi ya dola 3,400 za
Marekani.
Hiki ni kioja na ushamba mwingine. Ina nini hiyo simu? Inavaa chupi?
5.
Pete
mbili ni sawa lakini bado alipoongea na waandishi alikuwa amevaa
mapete mengine. Sasa yote ya nini?
6.
Dola za
Marekani zote hizo kwa safari ya vijijini ni za nini? Au alizitoa huko
huko?
7.
Fedha
za Tanzania nadhani ni sawa maana yake alihitaji kulipia gharama
kadhaa. Pia, kadi mbili za benki ni sawa na hata mabegi matatu ya nguo
si ajabu, kama alikuwa na safari ndefu na hata baraghashia mbili si
tatizo.
8.
Nyaraka
za serikali, hii ni fedheha kubwa kwa kuwa kama naibu waziri alipaswa
kujua jinsi ya kutunza nyaraka za serikali mara aingiapo
hotelini au popote pale. Huwezi kuziweka nyaraka nyeti hovyo hovyo
tu.
9.
Pasipoti mbili zote za nini? Alihitaji
kwenda nazo Morogoro za nini?
Huenda moja ni ya kidiplomasia na nyingine ya utumishi serikalini
ama ya kiraia, lakini za nini zote hizo?
10. Kwenye silaha hapa ni suala la uhalifu
kwa mujibu wa sheria zetu labda kama kuna maelezo mengine.
SMG ni silaha ya kivita, labda kama yeye
na polisi wa Morogoro wanamaanisha kitu kingine kwa kutumia maneno
"SMG".
Huu ni uvunjaji wa sheria na wala hakuna
haja ya kujiuliza kwamba anaogopa nini au analinda nini, mbona
ameshindwa kulinda mali alizoibiwa?
Ingeibiwa angekuwa amewaweka raia wengi
sana na hata polisi hataraini. Nashangaa wale waandishi hawakuuliza
mapema ili tupate maelezo. SMG?
Hii ninayoita element ya excessiveness
ni ulimbukeni wa kiafrika haswa kwamba sasa una madaraka, kwa hiyo
unataka kila kitu kijazane kwako tu kwa kuwa hela zipo na
"haki" ipo hata kama haikubaliani na sheria zetu.
Mavitu, makompyuta, mahela, masilaha,
mavinasa sauti, mapete, madude mengi tu - Swali ni je, kuna busara
hapo? Kuna utu-uzima hapo? Hii ni sifa nzuri ya kiongozi kweli
kujijazia mavitu hovyo hovyo tu na kuishiwa kuibiwa kirahisi namna
hii bila haya?
Lakini kutokana na utamaduni wetu wa
kulindana unaojengeka siku hizi, huyu hataguswa.
Hii ni aibu kubwa mno kwa taifa letu na
yeyote anayetetea mambo kama haya, hana nia njema na taifa
hili. Pana tatizo hapa, ni zaidi ya kuibiwa naibu waziri fulani.
Kwa maoni kuhusu makala hii (Gazeti la Tanzania Daima), wasiliana kwa simu +255
713260071
|
No comments:
Post a Comment