Rais Abdoulaye Wade ashindwa uchaguzi Senegal
Abdoulaye Wade.
Rais
Abdoulaye Wade wa Senegal amekubali kushindwa kwenye uchaguzi mkuu wa duru ya
pili nchini humo uliofanyika jana Jumapili. Wade alimpigia simu Rais mtarajiwa Macky
Sall kumpongeza kwa ushindi.
Sall
aliwahi kuwa Waziri Mkuu kwenye serikali ya Wade, wakashindana kiitikadi.
Kukubali
kushindwa kwa Wade ni hatua muhimu ya kidemokrasia barani Afrika, kwani ni aghalabu
sana kwa Marais waliopo madarakani kuachia ngazi hivi hivi bila rabsha!
Rais
wa kwanza wa Senegal; Léopold Sédar Senghor (9 October 1906 –
20 December 2001), alikuwa Rais wa
kwanza barani Afrika kujiuzulu akiwa madarakani, Desemba 1980.
No comments:
Post a Comment