Mbunge wa Jimbo la
Mtera Mh. Livingstone Lusinde akimwaga sera za Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika
Mkutano wa Kampeni uliofanyika Viwanja vya Ngarasero katika Kata ya USA River
Wilayani Arumeru. Mkutano huo ulifanyika tarehe 26/03/2012 majira ya saa 9
Alasiri.
10 comments:
CCM wanamjua huyu kuwa ni mtu wa aina gani. Hata alipoenda Arumeru walijua fika atazungumza nini.
Inasikitisha.
Sijasikia waliyosema CHADEMA, lakini kama ni kweli, siasa za Tanzania zinasikitisha kweli!
Duh! mtu mzima anatukana hivi?
Kiongozi kama huyu alipaswa ajibu kwa njia ya hoja ili ionekana CCM imekomaa kisiasa sasa hivi kama ni kweli anavyosema Chadema wanatukana sasa na yeye anatukana sasa wananchi tunawaonaji wote wapuuzi. Inamana mwendawazimu akikupiga wewe utapigana nae wote hamfai kuongoza hii nchi ndiyo maana nchi inaenda inakoelekea.
Ni kweli ndio maana nchi inakwenda mrama!
Ni aibu kubwa. Wakati anatoa matusi hayo ni watoto walikuwepo, kauchuna hana aibu hata kidogo. Halafu ni Mbunge huyu? Dah! Sielewi kuwa vyama vya siasa Tanzania vinaweza kutukanana kwa matusi ya nguoni kiasi hiki.
Pamoja na matusi yote haya CCM wameshindwa!
CCM tukae tukijua kuwa kuna vyama vya upinzani makini sasa si mchezo! Tuliwapeleka wazito wao wote tukaogopa kumpelekea mwenyekiti wetu Kikwete manaake ingekuwa aibu.
CHADEMA sasa onyesheni upevu angalieni makosa yenu jisahihisheni na nawatakia kila la heri.
Kama alivyosema Nape Mnauye baada ya matokeo kuwa asiyekubali kushindwa si mshindani.
Wana CCM tukubali tumezidiwa kete na CHADEMA Arumeru.
Tuwe makini na watu kama hawa wanaotukana saa zote. Ikiwezekana tuwaondoe. Kuna vijana wengi CCM wenye uwezo wa kuzungumza bila kutukana!!!
MwanaCCM Mdemokrasia wa kweli
Yaani nashangaa wamama wanatukanwa kwani kupata mimba ni dhambi nao kwakukosa elimu na uelewa wanamshabikia. Hawa ndo watu wanauwa CCM. CCM inakuwa kama chama cha mitaani tu. CCM tutumie akili hapa tunazidi kuivunja badala ya kuijenga. Watu wameeendelea sikuhizi. Mtu anatukanaje kwenye kadamnasi hivyo na kuachiwa huru. Kweli nchi haina sheria ni bora tu wapinzani iwe CAHDEMA au CUF wachukue tu uongozi kurekebisha nchi ime kufa kwishnei. Watu wengi tunajitoa CCM japo hatujui tunaenda wapi lakini kuliko niwe kwenye chama kimajaa matusi hivi bora kutojihusisha na vyama kabisa
Waanzishi wa ccm akina Marehemu Nyerere wangesikitika kuona lunateck kama huyu anawakilisha chama chao
Mmmmmmh!
Post a Comment