Aspirini inaweza kuzuia saratani
Kumeza kidonge cha aspirini kila siku
inaweza kuzuia na hata kutibu saratani. Taraifa hii ni kwa mujibu wa utafiti
mpya. Matokeo ya utafiti huo yalichapishwa na
jarida la matibabu la The Lancet, na hivyo kuzidisha kuonyesha manufaa ya
aspirini katika matibabu ya saratani.
Watu wengi
tayari wanatumia Aspirini kama dawa ya maradhi ya moyo. Lakini wataalamu
wanaonya kuwa hakuna ushahidi wa kutosha kuelezea watu kutumia aspirin ili
kuzuia saratani na hata vifo vinavyotokana na saratani.
Wataalamu hao wanaonya kuwa dawa hiyo inaweza kusababisha athari kubwa kama kuvuja damu tumboni.
Prof Peter
Rothwell,wa chuo kikuu cha Oxford akiwa na wakufunzi wengine ambao wamefanya
utafiti wa hivi karibuni, tayari walikuwa wamehusisha aspirin na kuzuia aina ya
saratani hasa saratani ya matumbo.
Vidonge vya Asprin
Lakini utafiti wao
wa awali, ulipendekeza kuwa watu wanahitaji kutumia dawa hiyo kwa takriban
miaka 10 ili iweze kufanya kazi hiyo.
Sasa wataalamu wanaamini kuwa uwezo wa dawa hiyo kuzuia saratani, hutokea mapema mno kati ya miaka mitatu na mitano. Hii ni kwa mujibu wa taarifa mpya kutoka kwa majaribio 51 yaliyohusisha wagonjwa 77,000.

Lakini
wakati kikundi cha wataalamu, kilichoongozwa na Profesa Rothwel kilidurusu
wangapi kati ya watu waliohusika katika utafiti huo walipata kuugua saratani na
hata kufariki kutokana na ugonjwa huo, waligundua kuwa vifo vilitokana pia na
matumizi ya aspirin.
Kuzuia kusambaa kwa Saratani
Kwa mtu anayetumia kiwango kidogo cha dawa hiyo kila siku, ilionekana kupunguza idadi ya visa vya saratani kwa robo baada ya miaka mitatu pekee.
Kuzuia kusambaa kwa Saratani
Kwa mtu anayetumia kiwango kidogo cha dawa hiyo kila siku, ilionekana kupunguza idadi ya visa vya saratani kwa robo baada ya miaka mitatu pekee.
Ni watu tisa
waliogungulika kuwa na saratani katika watu elfu moja kila mwaka ikilinganishwa
na watu kumi na mbili kwa watu elfu moja kwa wale waliomeza tembe hizo.
Pia
ilipunguza idadi ya vifo vilivyookana na saratani kwa asilimia kumi na tano.
ONYO - USITUMIE DAWA BILA USHAURI WA DAKTARI TAFADHALI SANA .
Habari hii kutoka BBC Kiswahili
ONYO - USITUMIE DAWA BILA USHAURI WA DAKTARI TAFADHALI SANA .
Habari hii kutoka BBC Kiswahili
No comments:
Post a Comment