Bingu wa Mutharika afariki dunia
Rais
wa Malawi Bingu wa amefariki dunia baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo, akiwa
na miaka 78. Duru kutoka kwa serikali zimethibitisha kifo hicho kwa BBC. Mwili
wa wa kiongozi huyo umepelekwa Afrika Kusini. Hata hivyo serikali haijatoa
taarifa rasmi kuhusu kifo cha Wa-Mutharika. Mmoja wa madaktari waliokuwa
wakimhudumia kiongozi huyo ameambia BBC, Wa-Mutharika alikufa baada ya moyo
wake kusimama.
Wadadisi wameonya kifo cha
rais huyo huenda kikazua mgogoro wa uwongozi. Katiba ya nchi inampa nafasi
Makamu wa Rais kuongoza nchi endapo Rais atafariki au kuugua kiasi cha
kushindwa kuongoza taifa.Hata hivyo Makamu wa Rais nchini Malawi, Joyce Banda
alitofautiana na Wa-Mutharika kufuatia mzozo wa urithi wa uongozi ambapo
alifukuzwa kutoka chama tawala,Democratic People's Party (DPP).
Kakake rais ambaye ni
Waziri wa mambo ya nje Peter Mutharika aliteuliwa kugombea urais hapo mwaka wa
2014.Mwandishi wa BBC mjini Blantyre Raphale Tenthani amesema mawaziri wamekuwa
na kikao usiku mzima kujadili hali ya sasa. Rubaa za serikali zimenukuliwa
zikisema kwamba maiti ya Rais imesafirishwa Afrika Kusini huku maafisa
wakitafakari hali ya sasa.
Bingu wa Mutharika
aliingia madarakani mwaka wa 2004. Baadaye alikihama chama chake cha United
Democratic Front (UDF) kwa tuhuma za wanachama kuhujumu harakati za kupambana
na ufisadi. Alichaguliwa tena mwaka 2009, lakini katika siku za karibuni
wakosoaji wake wamemlaumu kwa kuegemea sera za kiimla.
Rais huyo alikumbwa na
shinikizo za kuachia madaraka kwa tuhuma za kupendelea ukoo wake, na kuharibu
madaraka.Wa Mutharika aliwakera wafadhili wa kigeni hasa baada ya kumfukuza
balozi wa Uingereza Fergus Cochrane-Dyet, na kufanya utawala wa Uingereza
kusimamisha msaada kwa Malawi.
Chanzo:
BBC Kiswahili
No comments:
Post a Comment